Jumatatu 2 Juni 2025 - 17:46
Mtafiti wa Uingereza: Kadhia ya Palestina Imeonesha Kuwa Kanuni za Kimataifa Hazina Ufanisi!

Hawza/ Kwa mujibu wa Salman Sayyid kutoka Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza, kadhia ya Palestina ni mada inayohusu madai ya haki duniani kote leo hii.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika Mkutano wa Nne wa Utafiti wa Kiislamu uliofanyika mjini Istanbul, Uturuki, Bwana Salman Sayyid, mmoja wa watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Leeds, alieleza matumaini yake kwamba tukio hili litakuwa sababu ya kuimarika kwa mahusiano na mshikamano wa wanataaluma na watafiti duniani kote.

Alitaja kuwa lengo la kongamano hili ni kusafisha maarifa ya Waislamu kuhusiana na hali ya dunia ya sasa na kuchunguza uchambuzi unaotolewa.

Bwana Sayyid alisema: "Kile kinachotokea Palestina kina maana kwamba Waislamu hawakuweza kuwa na athari muhimu na ya haraka katika mabadiliko ya dunia, na hali hii inaonyesha kutofanya kazi kwa sheria za kimataifa, hasa kwa kuzingatia kwamba sheria hizi zinadaiwa zaidi kwa Waislamu."

Aliendelea kusema: "Iwapo leo hii hatuwezi kuwasimamia watu ambao mateso yao tunayashuhudia moja kwa moja kupitia runinga zetu kwa macho yetu wenyewe, na hatuwezi kupunguza mateso yao, basi hizi sheria za kimataifa na za kibinadamu zina faida gani? Hivi sasa Wapalestina wanashuhudia ukoloni wa kisasa wa Magharibi katika nchi yao."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha